Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amewezesha kununua magari 12 ya kisasa ya Zimamoto, yatakayotumika katika shughuli za uokoaji.
Bahungwa ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma hii leo Februari 3, 2025 na kuongeza kuwa na kwamba kwasasa wapo mbioni kununua Helikopta maalumu kwa ajili ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Amesema, “tayari Mheshimiwa Rais ameshatuwezesha tumenunua magari 12 ya kisasa. Lakini vilevile tuko mbioni kununua Helikopta maalumu kwa ajili ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.”