Mabadiliko ya Makocha ndani ya Yanga kwa siku za hivi karibuni yamemuibua aliyewahi kuwa msemaji wa klabu hiyo Jerry Muro akimtaka Rais Hersi Saidi kutoka hadharani na kutoa ufafanuzi wa nini kinaendelea klabu hapo ikizingatiwa timu inafanya vizuri kwa sasa.
Muro ameonekana kutofurahishwa na maamuzi ya viongozi ndani ya Yanga akihofia maamuzi  yasiyo sahihi yataifikisha klabu hiyo pabaya. Kuondoka kwa Gamondi baada ya kupoteza michezo miwili dhidi ya Azam na Tabora kuliibua maswali na hata alipoletwa Saed Ramovic wengi walihoji juu ya CV yake huko Afrika Kusini ambayo wengi wao waliiponda na kusema uongozi umekurupuka kwani Yanga ni klabu inayohitaji kocha mzoefu na mwenye CV kubwa Afrika.
Kocha Ramovic ameondoka Yanga baada ya siku 81 akiiongoza Yanga kwenye michezo 13 akishinda michezo 9 ya ligi kuu , CRDB CUP na Ligi ya mabingwa Ulaya . Kocha huyo hajapoteza mchezo wowote wa ligi kuu.
“Sipingani na mabadiliko waliyofanya viongozi ila tunachokiwaza sisi tunawaza zaidi kwa niaba yao na kuhoji baadhi ya vitu ambavyo havijapewa majibu kwa muda mrefu na hakuna kiongozi yeyote amethubutu kutoka na kuzungumza yale yote yaliyotokea na huku wanachama wanatamani kuyajua”
“Lakwanza kuondoka kwa Gamondi tulisikia tu watu wanaongea mara hafanyi vizuri wachezaji anawapeleka kwenye starehe mwisho akaondoka tukiamini viongozi wamekaa chini na kutafakari na kuona mtu gani sahihi anaweza kufaa wakamleta Ramovic lakini leo tunasikia huyohuyo kocha anaondolewa na kutangazwa mwingine hii inafikirisha kwamba wamemchunguza muda gani au alikuwepo kwenye makabrasha yao? ”
“Nimeomba viongozi wajitokeza sasa waongee na haswa Rais wa klabu huu sio wakati wa Ally Kamwe kuongea ni jambo kubwa kidogo, tunataka kumsikia Rais atoe neno aponye mioyo yetu maana ndio mfariji wetu”
🗣️ Jerry Muro – Msemaji wa zamani wa Yanga SC

Paul Pogba ahusishwa na Marseille wenyewe wamkataa
Coastal Union yawapa Dili Mama Lishe mkoa wa Tanga