Klabu ya Arsenal imeondolewa rasmi kwenye michuano ya Kombe la Ligi la Uingereza baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Newcastle. Huu ulikuwa mkondo wa pili wa nusu fainali ya michuano ambapo mkondo wa kwanza wa mchezo uliopigwa dimba la Emirates na Arsenal walifungwa mabao 2-0.

Mchezo uliopigwa dimba la St.James Park ulishuhudia Newcastle wakiendeleza ubabe wao kupitia kwa Jacob Murphy dakika ya 16 na Antony Gordon dakika ya 52.  Matokeo hayo yamewafanya Arsenal kuondoshwa kwenye michuano hiyo kwa jumla ya mabao 4-0.

Newcastle United wamefanikiwa kutinga fainali na sasa watamsubiri mshindi kati ya Tottenham au Liverpool mchezo utakaopigwa Dimba la Anfield tarehe 6 Februari baada ya mchezo wa kwanza Tottenham kuibuka na ushindi wa bao 1-0. Kama mchezo huo utaisha kwa sare yoyote ile Tottenham watatinga fainali na mchezo wa fainali dhidi ya Newcastle utapigwa Dimba la Wembley tarehe 16 March

Afya Tip: Sababu, Tiba ya viungo kufa ganzi
Masauni azindua Mradi wa utunzaji vyanzo vya Maji