Chelsea wana imani kuwa beki wa Crystal Palace na England Marc Guehi, 24, atajiunga nao badala ya kuelekea Tottenham msimu huu wa joto. (TBR Football)
Newcastle United inakadiria kuwa thamani ya mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak mwenye umri wa miaka 25 ni pauni milioni 150. (Fichajes – kwa Kihispania)
Chelsea iko tayari kumuuza kiungo wa Brazil Andrey Santos, 20, ambaye yuko Strasbourg kwa mkopo, mwishoni mwa msimu huu. (Team Talk)
Arsenal iliwafuatilia wachezaji wanne wakati wa usajili la Januari lakini ikaamua kutomsajili mchezaji yeyote kwa sababu hawakupata chaguo bora. (Mail)
Newcastle wamekataa ombi la Galatasaray kuhusu uhamisho wa beki wa Uingereza Kieran Trippier, 34. (Caughtoffside)
Manchester United, Chelsea na Newcastle wanavutiwa na mshambuliaji wa Crystal Palace na Ufaransa Jean-Philippe Mateta, 27, ambaye bado hajasaini mkataba mpya. (TBR Football)
Chelsea inatarajiwa kupunguza bei kiungo wa kati wa Uingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 26, baada ya mazungumzo ya uhamisho kufeli mwezi Januari. (Football Insider)
Manchester United wanatarajia kupunguziwa zaidi ya £27m kwenye tuzo yao ya Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu. (Football Insider)
Kuna kipengele cha pauni milioni 62 cha kumrumhusu mchezaji kuondoka katika mkataba wa miaka minne na nusu uliotiwa saini na mshambuliaji wa Wolves na Brazil Matheus Cunha wiki iliyopita, bila kujali ni klabu gani inaweza kutumia. (Mail Plus – usajili unahitajika)
Stuttgart wanavutiwa na kocha wa Como Cesc Fabregas kama meneja wao ajaye, iwapo Sebastian Hoeness ataondoka katika klabu hiyo ya Bundesliga msimu wa joto. (Bild, via Football Transfers)