Klabu ya Liverpool imeendelea kufanya vyema kwenye makombe mbalimbali inayoshiriki msimu huu. Ushindi wa mabao 4-0 walioupata dhidi ya Tottenham mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali kombe la Ligi la Uingereza (EFL) umeifanya Liverpool kufika fainali kwa wastani wa mabao 4-1 na sasa itakabiliana na Newcastle United mwezi machi 18.

Tathmini: Liverpool vs Tottenham

Kocha Arne Slot aliingia uwanjani akiwa na deni la bao 1 hivyo alipanga kikosi imara kilichoongozwa na mlinda mlango Kelleher,mabeki wakiwa ni Bradley,Konate,Van Dijk na Van Dijk. Eneo la kiungo liliundwa na Gravenberch,Jones na Dominik. Eneo la ushambuliaji liliongozwa na Nunez aliyezungukwa na Mohammed Salah na Cody Gakpo na mfumo thabiti wa 4-2-3-1.

Katika mchezo huo mzuri na kuvutia Liverpool walijipatia bao la uongozi kupitia kwa Cody Gakpo dakika ya 36 na kwenda mapumziko wakiwa na bao 1-0. Mohammed Salah ameendelea kufanya vyema baada ya kufunga bao la pili dakika ya 51 kwa mkwaju wa penati,Dominik alipigilia msumari wa tatu dakika ya 75 na Virgil Van Dijk akizamisha boti la Tottenham kwa bao lake la nne dakika ya 80.

Liverpool yazidi kuwa tishio 

Liverpool wamekuwa na msimu mzuri chini ya Kocha Arne Slot wakifanikiwa kufika kutinga hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa Ulaya wakiongoza msimamo wa ligi kwa alama 21 katika michezo 8 waliyocheza. Liverpool imeendelea kuongoza msimamo wa ligi kuu ya Uingereza kwa alama 56 kwenye michezo 23 waliyocheza mpaka sasa.

 

Serikali yatarajia kutoa waraka kwa Wakurugenzi wa Halmashauri
Tetesi za Usajili Duniani Februari 7,2025