”Barcelona ya sasa ukijichanganya tu unapigwa bao za kutosha”. Huu ni usemi wa mashabiki wa Barcelona wenye uhalisia ndani yake baada ya kuendelea kutoa vipigo kwa wapinzani wake. Barcelona imekutana na Valencia hatua ya robo fainali ya kombe la Copa Del Rey mchezo uliomalizika kwa Barca kushinda mabao 5-0.
Tathmini ya mchezo
Kocha Hans Flick ameendelea kuwasambaratisha wapinzani wake kwa kutumia mfumo pendwa wa 4-3-3 unaoundwa na Szczesny,Joule Kounde,Eric Garcia,Cubarsi,Balde,Lopez ,DeJong,Pedri ,Lamine ,Torres na Rafinha. Katika mchezo huo wa kuvutia Barcelona walipiga jumla ya mashuti 17 na mashuti 9 yalilenga golini na 5 kati ya hayo yalizaa mabao wakiwa na umiliki wa mchezo kwa asilimia 77.
Ferran Torres ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo akifunga mabao matatu dakika ya 3,17 na 30 mabao mengine yalifungwa na Fermin Lopez dakika ya 23 na Lamine Yamal dakika ya 59. Matokeo haya yanawafanya Barcelona kutinga nusu fainali ya Copa Del Rey wakiungana na Real Madrid, Real Sociedad na Atletico Madrid hivyo tutegemee upinzani mkali katika michezo katika hatua hizo