Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Wafanyabiashara kujiandaa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kufanya Biashara kwa Uadilifu na kuwa na Huruma kwa Wananchi.
Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Masjid Jibril Mkunazini alipojumuika katika Sala ya Ijumaa.
Aidha Alhaj Dkt.Mwinyi amesema kumekuwa na kawaida na tabia ya Baadhi ya Wafanyabiashara kupandisha bei Bidhaa wakati huo.
Amefahamisha Kuwa Serikali imekuwa ikipunguza Ushuru katika Mwezi wa Ramadhani hivyo si jambo jema kwao kupandisha bei za bidhaa na kuwaongezea mzigo Wananchi.
Akizungumzia suala la Uchaguzi Mkuu Ujao Alhaj Dkt, Mwinyi amewasisitiza Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi Kudumisha Amani ili Uchaguzi huo Ufanyike kwa Utulivu na Amani.
Wakati huo huo Rais wa Zanzibar Alhaj Dkt.Mwinyi amefika Jamati la Jumuiya ya Ismailia Aga Khan Kiponda na Kusaini Kitabu cha Maombolezo kufuatia Kifo cha Kiongozi wa Jumuiya hiyo Aga Khan wa Nne Prince Shah Karim Al- Husseini aliyefariki hivi karibuni Mjini Lisbon Ureno akiwa na Miaka 88.

Tunafanyia kazi maboresho ya Tozo kwa Wachimbaji wadogo - Mavunde