Na Johansen Buberwa – Kagera.
Serikali imeyataka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yanayofanya shughuli zake hapa nchini kuepuka kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki unapokaribia uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Mwantumu Mahiza ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya siku mbili mkoani Kagera ya kuzungumza na Viongozi wa mashirika hayo Manispaa ya Bukoba.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA0009-1024x713.jpg)
Amesema ni muhimu mashirika hayo yakafuata sheria kanuni na miongozo wakati Serikali kuu ikiagalia namna ya kufanya tahimini ya faida, hasara na changamoto wanazo kutana nazo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Hajjat Fatma Mwassa amesema wanatambua umuhimu wa mashirika hayo maana yamekuwa yakileta maendeleo kweye jamii zikiwemo shughuli za Afya, elimu na maji pamoja na kupinga vitendo vya ukatili.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA0013-1024x636.jpg)
Naye mdau wa maendeleo Dason Kateme kutoka Tumaini jipya ameyaomba mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuendelea kuilinda amani ya Taifa na kutotumika kisiasa hali ambayo inaweza kuhatalisha amani wakati Taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu.
Awali, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali, Makala Jasper amsema Mkoa wa Kagera una mashirika 219 ya Kitaifa 166 na Kimataifa manne na baraza hilo limeanza kuchukua hatua ya kubaini baadhi ya masharika ambayo yekuwa yakienda kinyume na utaratibu wa ufanyaji kazi hapa nchi.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250207-WA0017-1024x707.jpg)