Katika mpambano wa kustaajabisha katika Kombe la FA, miamba wa Ligi ya Premia Liverpool waliangushwa na timu ya daraja la pili Plymouth, wakipokea kichapo cha bao 1-0 ambalo lilizima matumaini yao ya kushiriki na kushinda makombe manne waliyokuwa wakiwania msimu huu.

Licha ya kuongoza Ligi ya Premia kwa pointi sita na kushikilia mchezo mmoja mkononi, harakati za Liverpool kusaka mataji makubwa manne ziligonga mwamba mzito walipoondoka kwenye kinyang’anyiro hicho mapema. Kampeni yao ya kuvutia ilijumuisha kutinga hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa na kufika fainali ya Kombe la Ligi ya Uingereza na kuongoza msimamo wa ligi ya Uingereza wakiwa na matumaini ya kutwaa ubingwa huo.

Tathmini  ya Mchezo

Kocha Arne Slot alifanya mabadiliko makubwa kikosini akiwapumzisha nyota wengi waliocheza mchezo wa nusu fainali na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tottenham kombe la ligi  ya Uingereza.Mbali na mabadiliko hayo Liverpool waliushika mchezo kisawasawa wakiongoza umiliki kwa asilimia 75 wakipiga mashuti 14 na 4 kati ya hayo yalilenga golini wakipiga jumla ya pasi 593.

Bao la Ryan Hardie kwa mkwaju wa penati dakika ya 53 lilizima mategemeo ya Liverpool na sasa watapambania makombe matatu wanayoshiriki. Kutinga fainali ya EFL kunaleta msisimko mkubwa inapokutana na timu ngumu ya Newcastle na fainali hiyo itapigwa machi 18

Mahusiano: Dkt. Pindi Chana atakiwa kufika Serengeti
Wapinzani wasiwatumie Vijana kufanya vurugu - Wasira