Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema kwamba chama chake kinamini kuunda serekali kwa
kutumia Falsafa Jumuishi ambayo haitabagua vijana wakizanzibari kutokana na itikadi na imani za vyama vyao tofauti vya siasa.

Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo viwanja vya Stela Daraja bovu Jimbo la Welezo wilaya
ya Maarib A Unguja alipohutubia wananchi na wanachama wa chama hicho katika mkutano wa hadhara akiwa mkatika mfululizo wa
mikutano ya kisiasa iliyopewa jina la bandika bandua yenye nia ya kuelezea mustakabali na umuhimu wa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka
huu wa 2025.

Amesema, Vijana hawapaswi kufanya makosa ya kutokiuna mkono chama hicho kwamba chama chake kinakusudia kuinyoosha nchi na kuwakabidhi vijana ili washindane katika kuipeleka mbele nchi yao kwa kuwa ubaguzi hauwezi kusaidia katika kujenga maendeleo ya taifa.

Othman ameongeza kuwa, ni muhimu kujenga utawala mwema utakaoheshimu maamuzi ya wananchi kwa kuwa ufalme wa nchi ni Wananchi wenyewe na kwamba ndio wenye maamuzi juu ya namna wanavyotaka nchi yao iendeshwe.

Amesema kwamba Zanzibar inazorasilimali nyingi za kiuchumi na pia imebahatika kuwepo katika eneo muhimu na zuri la kijerofia katika
kuendesha shughuli za kibiashara na kwamba inaweza kuleta mafanikio na kupia atua kubwa ya kimaendeleo kwa muda mfupi iwapo
itasimamiwa vyema.

Aliwataka wazanzibari katika uchaguzi ujao kutofanya makosa na kuhakikisha kwamba wanakiunga mkono chama ca ACT ili kuleta
mageuzi ya kweli kiuchumi na kisiasa na kuifanya Zanzibar kuwa na mamlaka yake katika kusimamia nyenzo zake za kiuchumi.

Ameongeza kuwa, kinachohitajika ni kuwepo uchaguzi huru na haki wenye ushindani wa Kidemokrsia na kuwataka wananchi wa Zanzibar
kukiunga mkono chama hicho ambacho kinakusudia kutetea haki za Zanzibar na kuchaia kasi ya maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake mwakilishi wa ngome ya wanawake kutoka mkoa wa Marib A kichama, Asha Mussa amaewataka vijana kuhakikisha kwamba wanakwenda kujiandikisha na kwamba wazazi wanawajibu wa kuwashajiisha watoto wao kufanya hivyo ili kuleta mageuzi ya kweli
muda wa uchaguzi utakapowadia.

Naye Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Chama hicho Nasro Amed Mazuri amewataka vijana kutambua kwamba wanawajibu na
jukumu kubwa katika kukiunga mkono chama hicho ili kufanikiwa kuleta mageuzi muihmu ya kimaendeleo yanayoitajika Zanzibar.

Kumbe kocha mpya wa Yanga anawajua JKT Tanzania nje,ndani
Rashford ameanza kwa kishindo Astonvilla