Wizara ya kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imeendelea kutekeleza mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao la pareto kwa kuhakikisha upatikanaji wa mbegu bora kwa wakulima katika maeneo yote yanayozalisha zao la pareto nchini ikiwemo Kisimiri Juu.

Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde ameyasema hayo hii leo Februari 10, 2025 Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, John Pallangyo aliyeuliza Je? Serikali ina mkakati gani wa kufufua Kilimo cha Pareto kisimiri Juu ili Wananchi wa eneo hilo wanufaike kama ilivyokuwa miaka ya 60 na 70.

Akijibu sali hilo, Silinde amesema, “COPRA kwa kushirikiana na Kituo cha Utafiti cha TARI Uyole imegawa bure kilo 890 za mbegu borakatika maeneo yanayozalisha Pareto ambapo Kisimiri Juu imepata kilo 100 ambazo zitapanda ekari 400.”

“Na kila ekari moja (1) ina uwezo wa kuzalisha kilo 450 za maua ya pareto. Aidha, ili kuwezesha wakulima kupata miche bora na mbegu hizo, zimekabidhiwa kwa Kampuni ya Pareto PCT kwa ajili ya kuzalisha miche ambayo itagawiwa kwa Wakulima wa Kisimiri Juu, na wakulima wapatao 300 wa Kisimiri Juu wamepatiwa mafunzo ya kilimo bora cha pareto ili waweze kulima zao hilo kwa tija,” amesema Silinde.

Hata hivyo amesema Wizara inaendelea kufanya tathmini kwa Vijana ambao wamepoteza kazi katika jimbo la alumeru mashariki kuhakikisha kwamba lileshamba linafufuliwa na kuweza kuajiri vijana hao.

“Kitu kikubwa ambacho niwathibitishia tu ni kwamba tunatambua shamba la oljoro alijatumika kwa muda mrefu na kuna wafanyakazi wamepoteza pale kazi kwa muda huu na hatma yao ni kwamba sisi Serikali tunatambua Hilo na tupo tunafanya tathmini ya lile shamba kuhakikisha linafufuliwa ili liweze kuajiri”, amesema

“Na kuhusu mpango kazi Upo tunauandaa ukikamilika tutakutaarifu Mbunge wa Jimbo Hilo na tutaongozana pamoja ili tuende tukafanye hiyo kazi kwa pamoja katika eneo hilo,“ amesema Silinde.

Serikali inatoa kipaumbele kufikisha Umeme Taasisi zinazotoa huduma kwa Jamii - Kapinga
Matajiri wa Ufaransa watangaza kumtaka Tchouameni