Real Madrid v Manchester City katika mechi ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa. Inakuwa mashindano ya kawaida ya nyakati zetu.Hii itakuwa mara ya nne kwa vinara hao wa soka kukutana barani Ulaya katika misimu minne iliyopita – lakini kukiwa na tofauti moja kubwa.

Wakati huu, badala ya kuwa katika hatua za mwisho, pande zote mbili zinapigania maisha yao ili tu kuingia 16 bora.Kwa hivyo ni vipi timu mbili zilizofanikiwa zaidi barani Ulaya katika misimu ya hivi karibuni zilishindwa kuingia nane bora na kuishia kwenye hatua ya mtoano?

Manchester City ipo  matatani msimu

Mara baada ya kushinda taji la Ligi kuu ya Uingereza kocha Pep Guardiola hakutaka kutumia bajeti kubwa kufanya maboresho kwenye kikosi chake.Maamuzi hayo yalifikiwa kutokana na  ukomo wa mkataba wake uliokuwa unamalizika mwaka 2025. Disemba 2024 kocha huyo aliongeza mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia City mpaka mwaka 2026.

Jambo hilo liliibua hisia miongoni mwa  Wadau wa soka wakiamini ujenzi uliofanywa na Guardiola kwa miaka 10 ulitosha kumpa heshima kwani ameshinda kila kikombe alichopata kushiriki.Kubwa zaidi ni namna gani angeweza kuondoka City msimu huu kwa heshima ya kipekee.

Kutofanya vizuri kwa City kumechangiwa na mengi  kwa msimu huu ,Moja ni umri wa baadhi ya wachezaji kama Kelvin De Bruyne,Walker,Gundogan umekuwa kikwazo kwa City.Pep amechelewa sana kupata mbadala sahihi kwa wachezaji hao.Kama kocha huyo angekuwa na mipango ya kudumu ndani ya City basi angehakikisha anaandaa timu ya vijana wenye ushindani mkubwa na kuleta mabadiliko stahiki.

Kwa mwenendo wa City inafikirisha kama itaweza kufanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya Real Madrid yenye wachezaji vijana na ubunifu wa kutosha.Si hayo tu lakini pia ushindani wa kumaliza nafasi nne za juu kwenye ligi umekuwa mkali haswa.Kuimarika kwa Arsenal ,Nottingham kunawafanya City watafute nafasi kwa wasiwasi .

Real Madrid na safu mbovu ya ulinzi

Real Madrid imekumbwa na changamoto kubwa msimu huu. Uwepo wa Vinicious jr,Mbappe,Rodrygo,na Bellingham umeifanya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kuwa tishio kwa wapinzani lakini eneo la ulinzi limekuwa tatizo kwao. Kukosekana kwa David Alaba limekuwa pigo kuu kwa klabu hiyo ya Uhispania na hilo limedhihirika katika mechi za hivi karibuni ambapo katika michezo dhidi ya Espanyol waliopoteza kwa bao 1-0, kushinda 3-2 dhidi ya Leganes na sare ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid

Kocha Carlo Anceloti atakuwa na kibarua kigumu jioni ya leo kuhakikisha timu hiyo hairuhusu mabao dhidi ya City.Matokeo chanya ya mchezo wa mkondo wa kwanza yatatoa tafsiri halisi ya mechi ya mkondo wa pili.

Ngoma awapagawisha waarabu ,Simba kuvuna zaidi ya bilioni 1
Tutashika dola kwa kura si Mtutu wa Bunduki - Wasira