Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM Bara, Stephen Wasira amesema katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 wataendelea kushika dola kutokana na wingi wa kura za Wananchi na si mtutu wa bunduki.

Wasira aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Busega mkoani Simiyu alipokuwa akielekea jijini Mwanza huku akieleza uimara wa CCM na kudai kuwa  CCM ni muungano wa vyama vilivyoleta ukombozi katika nchi uliotokana na vyama vya TANU na Afro-Shiraz Party (ASP).

Amesema, “katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, CCM tutashinda maana hakuna wa kupambana na sisi. Lengo letu ni kushika dola na dola hatuishiki kwa bunduki bali tunaishika kwa kura zinazopigwa na wana CCM na wasio wana CCM, kwa hiyo wanachama na viongozi wa Chama tunabeba maono ya vyama vilivyopita na sisi ndio tunaendeleza kazi ya uhuru na kuboresha maisha ya watu.”

“Wako watu wengine wako Ulaya na wengine wako hapa kama ‘maajenti’ wao, wanasema CCM imekaa sana nami nawauliza tulivyodai uhuru tulisema tutakaa mpaka lini? Tulidai uhuru kwa sababu kuna ajenda ya kubadili maisha ya watu, na kubadili maisha ya watu hakuna mwisho kwa sababu maendeleo yanazaa matatizo mapya,” alisema Wasira.

Ameongeza kuwa, “tunaendelea kujenga Tanzania yenye maendeleo kuondoa matatizo.Nataka kuwaambia Chama chetu ni kwa ajili ya kuwakomboa watu ambao hawana uwezo na hata wakipata matatizo hawawezi kuweka wakili, hivyo CCM ndio wakili wao. Tunataka Chama hiki kiwe wakili wa watu wote, tuwe tumaini la makundi yote, tunataka liwe tumaini la vijana wa Tanzania, tunataka liwe tumaini la Wafanyabiashara, Mama lishe na Wamachinga.”

Kuhusu wagombea ndani ya CCM hicho alisema tayari wameshapata wagombea wao wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, hivyo wanawasubiria watani zao(wapinzani)na kwa hali ilivyo katika vyama vyao Ikulu wataiona kwenye luninga.

“Mpaka hivi ninaposimama hapa hakijapatikana chama
mbadala wa kupambana na CCM hata CHADEMA imebakia nusu halafu watushinde. CCM ushindi ni lazima na ushindi unaotokana na kura.”

UEFA:Ni usiku wa vita kati ya Mbappe na Halaand
Baraza la Mawaziri la Kisekta EAC lakutana jijini Arusha