Raia 28 wanaoshukiwa kuwa ni wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia wamekamatwa na askari wa hifadhi ya Taifa Saadani katika eneo la bahari jirani na Kijiji cha Buyuni.

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Septemba 29, 2020 na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa TANAPA, Pascal Shelutete, ambapo amesema watu wamekuwa wakitumia hifadhi hizo kinyume na taratibu zilizowekwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, imeeleza kuwa tayari uongozi wa Hifadhi ya Taifa Saadani umewakabidhi washukiwa hao kwa Jeshi la Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

uongozi huo umetoa onyo kwa wale wote wenye dhamira ya kutumia Hifadhi za Taifa kuwa maeneo ya kufanya vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria na kwamba wasithubutu kufanya hivyo kwani wamejipanga vyema kukabiliana nao.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 30, 2020
Vigogo vyama vya siasa waitwa kwa msajili

Comments

comments