Johansen Buberwa – Kagera.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Kagera imefanikiwa kubaini uwepo wa vitendo vya rushwa katika Hifadhi ya Taifa Burigi Chato, viliyohusisa Askari polisi 13 ndani ya hifadhi hiyo baada ya kuwakodisha Wafugaji eneo la kufuga kinyume na sheria.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2024 Oktoba – Desemba kwa Vyombo vya Habari hii leo Februari 11, 2025, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kagera, Vangsada Mkalimoto amesema katika Wilaya ya Biharamulo baadhi ya Wafugaji waliwapatia Askari hao zaidi ya milioni 585.5 na Taasisi hiyo ilipokea taarifa na kuanza kufanya uchunguzi, ili kubaini ukweli.

Amesema, “TAKUKURU tulichukua hatua ya kuwasiliana na mwajiri wao ambaye ni TANAPA |aliyetoa ushirikiano mzuri na Askari hao waliitwa mbele ya kamati za maadili za TANAPA wakahojiwa na kupatikana na hatia na kuchukuliwa hatua na Askari watatu wamefukuzwa kazi na wanne wameshushwa vyeo huku sita wakipunguziwa Mshahara kwa asilimia 15 kwa kipindi cha miaka 13.”

Hata hivyo, Mkalimoto ametoa wito kwa Askari wanaofanya shughuli zao ndani ya Hifadhi kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kuacha kuruhusu Wafugaji kuingiza mifugo ndani ya Hifadhi ya Burigi huku akipongeza hatua zilizochukuliwa kwa wahusika waliokwenda na kinyume na sheria, ili iwe fundisho kwa wengine.

Dodoma jiji watoa taarifa rasmi ya kilichopelekea ajali
Mbogwe: Kituo cha mfano Katente chaongeza makusanyo