Ushindi wa mabao 3-0 walioupata Simba umewarudisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC.Shukrani za kipekee ziwaendee Jean ahoua aliyefunga bao la kwanza dakika ya 29 akimalizia pasi kutoka kwa Shomari Kapombe , Bao la pili liliwekwa kimiani na Ellie Mpanzu dakika ya 44 akipokea pasi kutoka kwa Lionel Ateba na bao la tatu liliwekwa na kimiani na Ladack CHASAMBI dakika ya 45+2 akimalizia v pasi kutoka kwa Shomari Kapombe.
Tathmini ya Mchezo
Kocha Fadlu Davies alianza na Camara ,Kapombe,Mohammed Husein ,Hamza ,Che Malone,Yusuf Kagoma ,Ladack Chasambi ,Fabbrice Ngoma,Lionel Ateba,Jean Charles Ahoua na Ellie Mpanzu akitumia mfumo wa 4-3-3. Matokeo hayo yanawafanya Simba kufikisha alama 47 na kupaa kileleni mwa msimamo wa ligi na wastani wa mabao 32 ya kufunga katika mechi 18 walizocheza
Matokeo ya Coastal Union vs Mashujaa.
Mashujaa wameshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa Lake Tanganyika baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na Coastal Union. Matokeo hayo yanawafanya Mashujaa kufikisha alama 20 katika michezo 18 waliyocheza na kupanda kutoka nafasi ya 11 mpaka ya 9 wakilingana alama na kuwashusha JKT Tanzania na Dodoma Jiji kwa tofauti ya magoli.
Klabu ya Coastal Union imepanda kutoka nafasi ya 7 mpaka ya 6 wakiwa na alama 22 sawa na KMC katika michezo 18 waliyocheza mpaka sasa.