Ligi ya Mabingwa Ulaya inaendelea leo usiku kwa mechi nane ngumu kuhakikisha zinapatikana timu nane bora zitakazofuzu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.Hizi hapa mechi ambazo hutakiwi kukosa na mechi ya kuvutia zaidi ni Real Madrid akivaana na Manchester City mchezo utakaopigwa Dimba la Etihad jijini Manchester nchini Uingereza majira ya saa 11 usiku.