Binti mmoja, Rabia Paulo (19) Mkazi wa Barabara ya Msalala, Kata ya Kalangalala, Wilaya ya Geita amekutwa amekufa kwa kujinyonga chumbani kwake baada ya kupata Divisheni Sifuri katika Matokeo ya Kidato cha Nne yaliyotoka hivi karibuni.
Akitoa Taarifa za matukio mbalimbali, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Sofia Jongo amesema tukio hilo limetokea Februari 11, 2025 majira ya saa 10 Jioni.
Amesema, Rabia alimsikia Mama yake akimuagiza mdogo wake aende akaangalie Matokeo ya Dada yake huyo ambapo mara baada ya maelekezo hayo, Binti huyo alijifungia chumbani kwake na kujinyonga.
Kufuatia tukio hilo, Kamanda Safia amewasihi Wazazi kuwa karibu na Watoto wao, ili kuweza kujua nyakati zao za furaha na huzuni na kwamba kinhefanyika kitendo kama hicho huenda kingeweza kuokoa maisha ya binti huyo.