Baadhi ya Viongozi wanaotekeleza majukumu yao kinyume na maadili Serikalini na kwenye Taasisi binafsi ni matokeo ya kukosa malezi bora kutoka kwenye familia zao pindi wakiwa watoto wadogo jambo linalopaswa kupigwa vita ili kuzalisha watendaji bora wnye kuzingatia maslahi ya wengi.
Hayo yamebainishwa February 13, 2025 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa Mkoa wa Pwani juu ya kaundika habari zinazohusu malezi na makuzi ya watoto na kubainika kuwa, ili kupata viongozi bora watakaolitumikia taifa kwa nyanja mbalimbali miaka ijayo jamii inapaswa kuongeza nguvu juu ya malezi i na makuzi kwa watoto hususa katika maswala ya elimu,afya na ulinzi..
![](https://dar24.com/wp-content/uploads/2025/02/d2a215d8-92e7-4384-a378-267ea12cb544.jpg)
Waandishi wa habari Mkoa wa Pwani, wakiwa kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuandika changamoto zinazowakabili watoto yaliyofanyika kwa siku moja Mjini Kibaha.
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku moja Mini Kibaha yameandaliwa na Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) na wakishirikiana na Taasisi inayojihusisha na maswala ya watoto yenye makao yake makuu Mkoani Pwani Anjita.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa ustawi wa jamii Mkoa wa Pwani,Eliah Kabola kutoka ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kibaha amesema kuwa suala la malezi na makuzi ya watoto linapaswa kushirikisha jamii nzima ikiwemo wazazi,walezi na wadau wengine.
“Watoto ndio viongozi wa kesho hivyo ni vema wakalelewa kwa kufuata misingi bora na hata kulindwa ili waje walitumikie taifa kwa kuzingatia maadili mema,” amesema.
Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka klabu za Waandishi wa Habari Nchini (UTPC), Victor Maleko amesema Viongozi bora wanajengwa kuanzia hatua ya chini hususa kwa kuzingatia malezi bora na makuzi.
“Waandishi wa habarii tunapaswa kuikumbusha jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia malezi na makuzi ya watoto ili kuzalisha viongozi bora watakaofanyakazi wakiwa na hofu jambo litakalosaidia kuleta msukumo wa mendeleo,” amesema.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Zablon Bugingo amesema kuwa iwapo jamii itashirikiana juu ya malezi na makuzi ya watoto si tu kuwa kutawezesha kupatikana kwa viongozi bora pekee bali hata kupata watu waliostaarabika na kukubalika kwa nyanja zote.