Msemaji wa Klabu ya Simba Ahmed Ally ameonekana kufurahishwa na maamuzi ya TFF kuwapeleka kamati ya maadili  wasemaji wa vilabu vya Yanga Ally Kamwe na Hamis Mazanzala wa Kagera Sugar. Kupitia mitandao yake ya kijamii Ahmed Ally ameandika

”Maafisa habari wa vilabu vidogo tambueni misingi ya kazi yenu,jueni mipaka ya kazi zenu ,Jifunzeni adabu na heshimu mamlaka, Kwa kifupi kuweni kama mimi”

Mashabiki waiponza Pamba

Mashabiki waliovamia uwanja mara baada ya mchezo kati ya Pamba na Azam uliomalizika kwa pamba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mashabiki walivamia uwanja na kuharibu taswira ya uwanja hivyo waandishi wa habari kushindwa kufanya mahojiano na makocha na wachezaji. Kupitia tukio hilo Pamba wameadhibiwa kulipa shilingi milioni 2.

Hii hapa taarifa kamili kutoka bodi ya Ligi

 

Tumejidhatiti kuboresha sekta ya Kilimo - Dkt. Biteko
Serikali yawataka Wananchi kutokata Miti Mlima Kilimanjaro