Mchezo wa Raundi ya 19 uliopangwa Februari 15 ukiwakutanisha Simba dhidi ya Dodoma jiji Feb 15 umeahirishwa na kusogezwa mbele na sababu kuu ni ajali ya basi waliyoipata wachezaji wa Dodoma jiji tarehe 10 Februari wakati wakitoka mkoani Mtwara kucheza na Namungo FC.
Kuahirishwa kwa mchezo huo kunawafanya Simba waendelee kusalia nafasi ya pili wakiwa na alama 47 katika michezo 18 waliyocheza. Mchezo unaofuata kwa Simba ni dhidi ya Namungo mchezo utakaopigwa Februari 19 katika uwanja wa Majariwa Stadium huko Ruangwa Lindi.
Hali ya wachezaji wa Dodoma jiji kwa sasa
Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za maendeleo ya wachezaji waliopata madhara kwenye ajali hiyo. Kuahirishwa kwa mchezo huo kutawafanya madaktari wa timu wawashughulikie wachezaji wao pamoja na benchi la ufundi
Uongozi wa Dar24 unatoa pole kwa wote waliofikwa na kadhia hiyo