Mshambulizi wa Manchester United Muingereza Marcus Rashford, 27, ambaye yuko kwa mkopo Aston Villa, hajakata tamaa ya kujiunga na Barcelona msimu huu wa joto. (Sun)

.

Atletico Madrid wanavutiwa na mshambuliaji wa Crystal Palace Mfaransa Jean-Philippe Mateta, 27, ambaye thamani yake ni pauni milioni 42. (Fichajes – in Spanish)

Manchester City wamembaini kiungo wa kati wa Atalanta na Ubelgiji Charles de Ketelaere, 23, kama mbadala wa Kevin de Bruyne, 33. (TBR Football)

Chelsea wako tayari kutoa mkataba wa pauni 83m kwa beki wa Ufaransa wa Barcelona Jules Kounde, lakini Klabu ya Uhispania haitaki kumuuza mchezaji huyo wa miaka 26 na ina mpango wa kumpa mkataba mpya. (Diario Sport – in Spanish)

Ajax wanatumai kuwasajili beki wa pembeni wa Brighton wa Ghana Tariq Lamptey mwenye umri wa miaka 24 na mlinzi wa Uholanzi Joel Veltman mwenye umri wa miaka 33 kwa uhamisho wa bure mikataba yao itakapokamilika msimu huu wa joto. (Mirror)

,

Arsenal wamewasiliana na Atalanta kuhusu uwezekano wa kumnunua mshambuliaji Mateo Retegui, lakini The Gunners wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka kwa Manchester United kumnunua mshambuliaji huyo wa Italia, 25. (CaughtOffside)

Liverpool wanataka kumsajili beki wa Tottenham na Uholanzi Micky van de Ven, 23, msimu huu. (Football Insider)

.

Chanzo cha picha,Getty Images

Al-Nassr na Al-Hilal wanamwinda mshambuliaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 28 Luis Diaz, ambaye pia anafuatiliwa na Barcelona. (Todofichajes – in Spanish)

Idara ya kuwabaini na kuwasajili wachezaji ya Manchester United yenye watu 80 inatazamiwa kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kama sehemu ya kufuta wafanyakazi 200 ili kupunguza gharama. (Guardian)

Slot afunguka sababu za kumtoa Konate mchezo dhidi ya Wolves
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Februari 17, 2025