Arne Slot amekiri kwamba alimtoa Ibrahima Konaté wakati wa mapumziko dhidi ya Wolves ili kumuepusha beki huyo wa Liverpool kupokea kadi ya pili ya njano, huku viongozi hao wa Premier League wakipata ushindi mnono kwenye Uwanja wa Anfield.Liverpool wamwwendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba dhidi ya Arsenal;

Luis Diaz aliipa Liverpool bao la uongozi dakika ya 15 na Mohammed aliandika bao la pili dakika ya 37 kwa mkwaju wa penati. Bao la kufutia machozi la kwa Wolves liliwekwa kimiani na Matheus Cunha dakika ya 67. Mchezo ulimalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa bao 2-1 na kufikisha alama 60.

Slot afafanua sababu za kumtoa Konate

kocha mkuu wa Liverpool, alifafanua: “Nilimwona akipata njano yake ya kwanza, ambayo kwangu ilikuwa laini. Ikiwa angepokea nyingine kwa kusukuma begani ambayo ingekuwa tena njano laini ingesababisha atolewe nje kwa kadi mbili za njano laini. Naamini mwamuzi alihisi hivyo hivyo.

“Hata hivyo, nimeona soka mara nyingi maishani mwangu na ninajua kwamba mchezaji na mwamuzi wote wako kwenye presha. Kwa hivyo, faulo inayofuata inaweza kumfanya mwamuzi kufikiria labda atoe. Ni ngumu sana kucheza dakika 45 dhidi ya timu yenye nguvu ya Wolves, kwa hivyo ilibidi nimtoe Ibou kwa sababu huwezi kucheza mpira ukiwa na mawazo kwamba huwezi kufanya faulo dhidi ya wachezaji wazuri kama wa Wolves.

 

United na PSG zaingia vitani kumsaka mkali wa kucheka na nyavu
Tetesi za soka Duniani Februari 17,2024