Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari, 2025 hadi Februari 2025 lilifanya operesheni dhidi ya uhalifu na wahalifu na kufanikiwa kuwakatama watuhumiwa wa makosa ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia 15 na kuwafikisha mahakamani, ambapo kati yao 10 walikuwa na tuhuma za ubakaji na wengine watano wa ulawiti.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamjzi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema baada ya kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za ubakaji, Watuhumiwa watatu walihukumiwa vifungo vya maisha Jela na mmoja kifungo cha miaka 30 jela.

“Aidha mtuhumiwa 01 amehukumiwa kifungo cha maisha jela na mwingine 01 kifungo cha miaka 30 kwa tuhuma za ulawiti. Watuhumiwa wengine kesi zao zipo katika hatua mbalimbali. Kupitia misako dhidi ya dawa za kulevya walifanikiwa kukamata Watuhumiwa 26 wakiwa na Mirungi Kilogramu 196.4, Watuhumiwa 22 wakiwa na Bhangi kilogramu 32 pamoja na kuteketeza zaidi ya hekari 10 za bhangi,” ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa, watuhumiwa wote wa Dawa za kulevya tayari wamefikishwa Mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali, huku upande wa mapambano dhidi ya ujangili, wakifanikiwa kukamata watuhumiwa wawili wakiwa na nyama ya Nungunungu kilogramu 20, ambapo tayari wamefikishwa Mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.

Sambamba na hayo amesema kuwa kwa kipindi hicho walifanikiwa kukamata Watuhumiwa 38 wakiwa na pombe ya Moshi lita 172 na mitambo minne ya kutengenezea pombe hiyo ambapo watuhumiwa wote tayari wameshafikishwa Mahakamani kwa taratibu za kisheria huku watumiwa 202 wa makosa ya wizi wakikamatwa katika operesheni hiyo.

Hiki anachonya Kim Jong un ni ukatili kwa wapenzi wa soka Korea Kaskazini
Vita mpya yaibuka baina ya Ronaldo na Benzema nchini Saudi Arabia