Ligi kuu ya NBC inaendelea jioni ya leo kwa mchezo mkali unaowakutanisha wakali wa Top Four Young Africans wanaoongoza ligi kwa alama 49 dhidi ya Singida Black Stars wenye alama 39 wote wakiwa wamecheza michezo 19. Mchezo huu ni muhimu kwa pande zote ili kuendelea kujiimarisha kwenye nafasi zao ,Yanga amepishana kwa alama 2 na mpinzani wake Simba mwenye alama 47 na mchezo mmoja mkononi wakati Singida atapaswa kushinda ili kupunguza wingi wa alama kwa mshindani wake Azam mwenye alama 37 mpaka sasa.

Mipango ya Mwalimu wa Yanga 

Licha ya Aziz ki kuwa na matukio ya kulipa mahali na kufunga ndoa wikiendi iliyopita na mlimwende Hamisa Mobetto. Hali ni tofauti kwa kocha Miloud Hamdi ambaye hajataka mchezaji huyo kwenda Honey moon na badala yake amempanga kwenye kikosi kitakachoivaa Singida Black Stars.Wengi tulidhani shamrashamra za Aziz ki zingemfanya cocha Hamdi ampumzishe na nafasi yake kuchukuliwa na Chama,Duke Abuya au Pacome lakini mambo ni tofauti.

Kocha huyo hajafanya mabadiliko yoyote kwenye kikosi akiwaanzisha nyota wale wale walioipa Yanga ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya KMC ambao ni Djigui Diara ,Israh Mwenda ,Shadrack Boka ,Dickson Job,Ibrahim Bacca Hamad,Khalid Aucho,Maxi Nzengeli,Mudathir Yahya,Prince Dube,Aziz Ki na Clement Mzize.

Kocha huyo amenukuliwa akisema ;

“Tumejiandaa kama ambavyo tumejiandaa mchezo uliopita. Tunafahamu ni mchezo mgumu na muhimu hivyo tumeongeza umakini mkubwa.Mchezo uliopita tulikuwa mchezo mzuri sana dhidi ya KMC FC, mpango wetu ni kucheza vile vile isipokuwa tunapaswa kuwa makini zaidi”

”Tunafahamu Singida ni timu nzuri sana ina wachezaji wenye ubora wa hali ya juu, lakini ni matumaini kuwa tutakuwa na mchezo mzuri uwanjani.

Nitaangalia vitu gani napaswa kubadilisha kwenye kikosi changu. Utakumbuka hatukucheza vizuri dhidi ya JKT lakini Singida wao walishinda, huo ndio mpira wa miguu. Hata hivyo mimi sio muumini mkubwa wa takwimu zilizopita. Unaweza kuwa na mchezo mzuri leo kesho ukawa na mchezo mbaya”

“Wanaonifahamu wanajua namna gani nina kuwa na uchu wa kupata ushindi, lakini hilo haliondoi ukweli kwamba tunapaswa kuwaheshimu wapinzani.Nikisema nawaheshimu wapinzani haimaanishi nina hofu, namaanisha mpira ni mchezo wa ushindani na kila mtu anatumia mbinu mbalimbali kujaribu kushinda hivyo lazima niende kwa tahadhari na umakini hata kama nahitaji kupata alama tatu”

Trilioni 8.2 zatumika kugharamia mikopo Elimu ya Juu
Arusha :Maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Samia Suluhu yanaridhisha