Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri amesisitiza umuhimu wa umoja na ushirikiano baina ya Taasisi za Sekta ya Maji Morogoro ili kwa pamoja ziweze kukabiliana na changamoto za huduma za maji na kuhakikisha huduma bora za Majisafi na Usafi wa Mazingira zinawafikia Wananchi.
Amebainisha hayo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Taasisi za Sekta ya Maji Morogoro katika kikao kilichofanyika leo Februari 17, 2025 kwenye ukumbi wa Bonde la Wami Ruvu.
Kwa upande wa viongozi na watendaji kutoka Sekta ya Maji Morogoro wameahidi kutekeleza maelekezo na maagizo yote yaliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
Taasisi za Sekta ya Maji Morogoro zilizoshiriki kikao hicho ni pamoja na Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA), RUWASA Morogoro na Maabara ya Ubora wa Maji Morogoro.

EWURA ihakikishe mafuta yanapatikana kwa gharama halisi - Dkt. Biteko
Habari kuu katika Magazeti ya leo Februari 18, 2025