Ndege ya Delta Air Lines iliyokuwa na watu 80 imeanguka katika uwanja wa ndege wa Toronto, na kuwaacha takriban watu 18 wakiwa wamejeruhiwa lakini hakuna vifo.
Ndege hiyo ya Endeavor Air 4819 iliyokuwa na abiria 76 na wafanyakazi wanne ilikuwa ikitua alasiri katika mji mkuu wa Kanada, ikiwa imesafiri kutoka Minneapolis katika jimbo la Minnesota Marekani.
Taarifa ya Huduma za wauguzi ilieleza kuwa kati ya watu 17 waliojeruhiwa watatu wana hali mbaya ambao ni mtoto mmoja, Mtu mzima mwenye umri wa miaka 60 na mwanamke mwenye umri wa miaka 40.
Mkuu wa huduma ya Afya, Lawrence Saindon amesema waliojeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wale walio na majeraha madogo, walipelekwa katika Hospitali za eneo hilo kwa ambulensi na helikopta.
Hakuna maelezo ya chanzo cha ajali hiyo yaliyotolewa, ingawa inadaiwa kuwa imetokea baada ya uwepo wa upepo mkali ulioripotiwa katika Jiji la Toronto