Mahakama ya Wilaya Sengerema Mkoani Mwanza, imemhukumu kwenda jela miaka mitatu Mkazi wa Kijiji cha Soswa Wilayani humo, Amos John Malaki  (30), baada ya kukutwa na hatia ya kuwang’ata na kuwajeruhi watu wawili. Mshtakiwa huyo, alifikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka hayo katika kesi hiyo ya Jinai namba 4079/2025 na kwa hiari yake amekiri kutenda makosa ya kuwajeruhi watu hao wawili. Akisoma mashtaka hayo Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Nyamhanga Tissoro alieleza kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Januari 8, 2025, Saa 5: 57 usiku kwa kumng’ata Regina Thomas kwenye jicho. Katika tukio lingine lililotokea Januari 9,2025 Saa 6:01 usiku, mshtakiwa alimng’ata kidole gumba cha mkono wa kulia, Mashaka Idd Daudi aliyefika kuamua ugomvi kinyume na vifungu vya 225 cha sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.
Amos Malaki ametiwa hatiani na Mahakama hiyo baada ya kupitia vifungu vya sheria na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri zikiwemo PF3 za wahanga baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu pamoja na maelezo ya kukiri ya mtuhumiwa wakati akihojiwa kituo cha polisi ambayo pia hakuyapinga mahakamani yalipotolewa kama kielelezo, mahakama imejiridhisha bila ya kuacha shaka kwamba mtuhumiwa  alitenda makosa hayo licha ya ukili wake. Akijitete Mahakamani hapo, mshtakiwa alisema kilichopelekea tukio hilo ni ulevi wa Pombe na kwamba mhanga wa pili aliingilia ugomvi usiomhusu baada ya kuona anagombana na mpenzi wake. Aidha, mshtakiwa pia aliiomba Mahakama imuachilie huru kwa kuwa ni mkosaji wa mara ya kwanza na kudai kuwa alisababishiwa na ulevi lakini Hakimu Kisoka alisema amemhukumuadhabu hiyo, ili iwe fundisho kwa wengine.

Wahusika tukio la ukatili kwa mwanamke waadhibiwe - TAMWA ZNZ
Maisha: Bila mbinu hizio afya yangu sijui ingekuwaje hii leo