Manchester United wanamtaka mshambuliaji wa timu ya vijana ya England chini ya miaka 21 kutoka Ipswich Town, mwenye thamani ya Pauni milioni £40m, Liam Delap mwenye miaka 22. Delap, ambaye alitoka timu ya vijana ya Manchester City, ambaye amefunga mabao 10 katika ligi kuu ya England msimu huu na pia anaswakwa na Chelsea pia. (i Paper), external

Liverpool iko tayari kumtoa mshambuliaji wake Mruguay, Darwin Nunez, 25, pamoja na fedha, ili kumnasa mshambuliaji Msweden, Alexander Isak, 25, kutoka Newcastle, ambaye ana thamani ya pauni milioni £40m100m. Isak amefunga mabao 17 kwenye ligi kuu England msimu huu. (Football Insider)

Hata hivyo, Newcastle haitaruhusu wachezaji wake huyo bora kuondoka iwapo hawafanikiwi kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. (Daily Mail)

Alexander Isak

Arsenal na Chelsea wanavutiwa na mshambuliaji wa Ufaransa anayekipiga Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, 22, kama mbadala wa Isak. (CaughtOffside)

Liverpool inamuania pia kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi, Frenkie de Jong, 27, ikimuweka kwenye orodha ya wachezaji ambao Reds inawataka kuwasajili kwenye dirisha lijalo la majira ya joto. (Teamtalk)

Meneja wa Bournemouth, Andoni Iraola, ambaye amewafanya mashabiki wa timu hiyo kuwa na ndoto za kushiriki michuano ya Ulaya, yupo kwenye orodha ya makocha wanaosakwa na Tottenham iwapo wataamua kumtimua Ange Postecoglou, ambaye amekuwa akiinoa timu hiyo tangu Juni 2023, lakini yupo kwenye kuti kavu kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo. (Talksport)

 Andoni Iraola

Chanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Andoni Iraola

Kiungo kutoka Argentina wa Manchester City, Maximo Perrone, 22, anayecheze Como kwa mkopo anataka kuhamia moja kwa moja kwenye timu hiyo ya Italia – inayoongozwa na mchezaji wa zamani wa Arsenal na Chelsea, Cesc Fabregas. (Calcioline – in Italian)

Kiungo wa kati ya wa AC Milani, Mholanzi Tijjani Reijnders, 26, atasaini mkataba mpya kusalia katika klabu hiyo ya Italia hadi mwaka 2030. (Fabrizio Romano on X)

Ahoua hana maisha marefu ndani ya Simba
REA kusambaza Mitungi ya gesi 16,000 Simiyu