Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dr es Salaam, imeamuru kutolewa kwa amri ya Mwanasiasa Mkongwe, Dkt. Wibroad Slaa (76) kufikishwa mahakamani ifikapo Machi 4, 2025 ili uweze kutolewa uamuzi wa kesi hiyo itakuwa inasikilizwa kwa njia gani.

Hakimu Mkazi Mkuu, Ushindi Swalo ametoa uamuzi huo Mahakamani hapo, ambapo awali Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema alidai kuwa shauri hilo lilipelekwa kwa ajili ya kutajwa na kueleza kuwa kwa kuwa shauri hilo lipo katika taratibu nyingine za kirufaa zinaendelea katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, hivyo aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya shauri hilo kutajwa.

Mkurugenzi wa Mashitaka alikata rufaa juu ya uamuzi huo uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam wa kuamuru shauri namba 993/2025 kurudishwa mahakamani hapo ili liweze kutolewa uamuzi juu ya dhamana ya Dkt. Slaa ambayo hapo awali iliwekewa pingamizi na upande wa mashitaka.

Aidha, Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili, Melkion Sanga ulidai kuwa katika kikao kilichopita ilitolewa amri ili mshitakiwa aweze kufikishwa mahakamani siku ya leo na kujua mwenendo wa kesi yake inavyoendelea.

Alisema, kwa kuwa mshitakiwa hakufikishwa aliiomba Mahakama itoe ahirisho fupi ili aweze kufikishwa Mahakamani kama ilivyoamuriwa katika kikao kilichopita, pia alidai kuwa amri ya mahakama ilivyotolewa ilitakiwa ifuatwe kwa mshitakiwa kufikishwa mahakamani hapo.

Akijibu hoja hiyo, Mrema alidai kuwa kwa upande wa mashitaka hawakupokea amri ya mshitakiwa kufikishwa kutoka mahakamani ndiyo sababu walishindwa kumfikisha mshitakiwa mahakamani hapo.

Alisema kwa mshitakiwa kufikishwa mahakamani hakuthibitishi afya yake ipo vipi kama alivyodai wakili wake, hivyo alidai kuwa mahakama inaweza kutoa uamuzi kwa kutoa amri mshitakiwa afikishwe mahakamani au kesi isikilizwe kwa mkutano wa njia ya video.

TANESCO kuboresha kituo cha kupokea, kusafirisha Umeme Ubungo
Maendeleo ya Takehiro Tomiyasu ni pigo kwa safu ya ulinzi ya Arsenal