Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limefanikiwa kudhibiti maandamano ya wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo February 19, 2025 katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza hasa katika wilaya ya Ilemela na Nyamagana.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP. Wilbrod Mutafungwa amesema maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika hayakuwa na uhalali wa kisheria hivyo Polisi walijipanga kuyadhibiti kwa kufanya doria maeneo mbalimbali ya jiji.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Said Mtanda amewataka wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, pamoja na Wananchi kutii sheria na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama ili kufanikisha uchunguzi na upatikanaji wa mwanachama huyo anaedaiwa kupotea tarehe 14.2.2025 ; na kwamba serikali ipo macho kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unakuwa salama.
Katibu wa CHADEMA mkoa wa Mwanza, Boniphace Nkobe amewataka wanachama wa CHADEMA kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la polisi na Serikali ili kuhakikisha mwanachama wao anapatikana akiwa salama.