Chelsea kushindana na vilabu vingine vya ligi kuu England ili kumnasa mlinzi wa England anayechezea Crystal Palace, Marc Guehi ambaye anathamini ya £70m. Mchezaji huyu mwenye miaka 24 alijiunga na Palace akitokea Chelsea mwaka 2021. (Mirror)
Liverpool na Manchester City zinamtaka beki wa kulia wa Bayer Leverkusen, Jeremie Frimpong, ambaye ana “makubaliano maalmu” na klabu yake hiyo ya Ujerumani kusikiliza ofa zinazofikia euro milioni 40 (£33.1m). Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, mwenye miaka 24, alikuwa katika timu za vijana za Manchester City kabla ya kuhamia Celtic mwaka 2019. (Team Talk)

Arsenal wana matumaini ya kumnasa kiungo wa kati wa Real Sociedad na Hispania, Martin Zubimendi, mwenye umri wa miaka 26, ambaye aliamua kubaki na klabu yake badala ya kujiunga na Liverpool majira ya joto yaliyopita. (Team Talk)
Mlinda lango wa timu ya Liverpool kutoka Jamhuri ya Ireland, Caoimhin Kelleher, 26, bado ni chaguo kuu la Chelsea msimu huu wa majira ya joto, the Blues wako tayari kutoa £40m kumsajili kipa huyo namba mbili wa Liverpool. (Football Insider)
Winga wa Barcelona kutoka Hispania, Lamine Yamal, 17, amevunja tetesi kwamba anahamia Paris St-Germain, akisisitiza mapenzi yake ya kusalia Barcelona. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia anayekipiga Liverpool, Luis Diaz, 28, anataka kusaini mkataba mpya na klabu hiyo licha ya kwamba mkataba wake wa sasa bado una miaka miwili kabla ya kumalizika. (TBR Football)
Klabu za Leicester City na Crystal Palace zinamfuatilia mshambuliaji wa Midtjylland na Guinea-Bissau, Franculino Dju, 20, ambaye alitokea katika timu za vijana za Benfica. (Bold – in Danish), external
Mchezaji wa zamani wa Fulham, Arsenal, na West Ham, Luis Boa Morte, ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Guinea-Bissau, anaonekana kuwa na shauku ya kuchukua nafasi iliyo wazi kuionoa Blackburn Rovers. (Sun)