Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso leo FFebruai 22, 2025 amefanya mabadiliko ya kiutendaji katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA)
Waziri Aweso kwa Mamlaka aliopewa na Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Na. 5/2019 amemteua CPA Sais Andongile Kyejo kuwa Mkurugenzi Mtendaji MORUWASA.
Kyejo alikua ni Mkurugenzi wa Fedha Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam – DAWASA, na atachukua nafasi ya Eng. Tamimu Katakweba aliekua Mkurugenzi Mtendaji wa MORUWASA.
Aidha Waziri Aweso amemuelekeza katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri kuunda timu maalumu ya Wataalamu watakaofanyia kazi changamoto za hali ya huduma ya upatikanaji wa Maji Manisapaa ya Morogoro na maeneo yote yanayohudumiwa na MORUWASA katika kipindi ambacho utekelezaji wa Mradi mkubwa wa Maji unaendelea.