Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis bado yuko katika hali mbaya baada ya vipimo vya damu kuonyesha dalili za kushindwa kwa figo.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 88, hakupata matatizo zaidi ya kupumua tangu Jumamosi na bado anapatiwa oksijeni kwa kiwango cha juu akikabiliwa pia na homa ya mapafu.

Vipimo vya damu, pia vimeonesha dalili za awali za kushindwa kwa figo ingawa jopo la Madaktari wanaomtibu wamesema hali hiyo inadhibitiwa.

Tayari waumini wa Dhehebu hilo na watu mbalimbali Duniani wanaendelea na maombi maalum katika Makanisa kwa ajili ya kumuombea afya njema.

Rais Samia katika hafla ya Uzinduzi wa Jengo la Halmashauri Bumbuli
Yanga wanapeta tu kileleni, Simba na Azam kupasuana leo