Johansen Buberwa – Kagera.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti Tanzania (ALAT), Murushid Ngeze amewaasa Wananchi kuacha tabia ya kuwakimbia watu waliopata matatizo kwani ni jambo ambalo haliepukiki na ni vyema kuukabili mthiani huo wa kimaisha.
Ngeze ameyasema hayo katika dua maalum iliyoandaliwa na familia yake kutoa shukran na iliyofanyika kata Rukoma Halmashari ya Bukoba Mkoani Kagera, ikihusisha Viongozi wa dini, Viongozi wa Kiserikali pamoja na Wananchi.

Amesema, “inabidi kujiepusha na desturi ya kuyakimbia matatizo kipindi yanapotokea kwa kujitenga na mtu aliyepata matatizo kwa hapa duniani kwa kila mmoja amepangiwa njia yake uwezi jua kila mtu amepangiwa wapi.”
Aidha, Ngeze ameongeza kuwa, “leo mimi atanipatia mtihani wa kuondokewa na kiungo na sijuhi safari bado ipo inaedelea cha msingi ni kukubali hali yoyote ile uliyonayo ukiwa imara shukuru mungu na kubaliana na hali hiyo ukuwa umeshapata matatizo kubaliana na hali hiyo.”

Katika hatua nyingine Ngeze amemshukuru Rais Dkt Samia Hassan pamoja na wasaidizi wake kwa juhudi zake za kugharamia matibu yake ndani ya nchi na nje ya nchi tangu amepata ajali Desemba 2022 iliyopelekea kuvunjika mguu wake mmoja hadi kukatwa na kupelekea kutembea kwa kutumia mguu bandia.
Mkuu wa Wilaya Bukoba Erasto Sima aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa amesema Kata ya Rukoma imekuwa mfano katika shughuli mbalimbali za maendeleo kupitia Mwenyekiti Ngeze, ambaye amekuwa chachu ya kusimamia miradi inatekelezwa kwenye halmashauri hiyo yenye vijiji 94 kata 29.

Baadhi ya Viongozi wa dini waliongoza dua ni pamoja na Mchungaji Mathias Buberwa wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kaskazini Magaribi, Padre Achileus Rugemalia Poroko Ichwandimi pamoja na Sheikh Twahir Said wa Wilaya Bukoba.
Kwa pamoja wameliombea Taifa la Tanzania liendelee kuwa na amani umoja na mshikamano, ili viongozi wake wajaliwe hema na busara katika kutekeleza majukumu yao kuanzia vitongoji hadi taifa na kuliepusha na migogoro mbalimbali.