Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amefanya ziara na kukagua ujenzi wa jengo la utawala shule ya Sekondari Komoto wenye gharama ya shilingi milion 122, iliyopo Kata ya Bagara Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoa Manyara na kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuacha tabia ya kuwadanganya Viongozi.

Akiwa kwenye ziara hiyo Sendiga ameagiaza kukamilishwa kwa ujenzi wa jengo hilo la utawala ifikapo Juni 16, 2025 ambapo utekelezaji wake ulianza mwaka 2021.

Sendiga pia amekagua ujenzi wa vyumba viliwili vya madarasa na chumba cha Ofisi katika Shule ya Msingi Darajani iliyopo Kata ya Maisaka Halmashauri ya Mji wa Babati na amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kukamalisha ujenzi huo mapema na kuacha tabia ya kuwadanganya Viongozi.

“Ninapo kuja sehemu tayari ninataarifa hii tabia ya kusikia kiongozi anakuja sehemu ndipo mnaleta mafundi ili mradi uonekane unaendelea kufanya kazi sio tabia nzuri, lengo la kuja ni kujua changamoto ni nini na mradi unakwama wapi ili Serikali tuweze kutatua changamoto hizo,” amesema Sendiga.

Handeni, Kilindi kupata Umeme wa uhakika
Tanga: Rais Samia azindua Shule ya Sekondari ya Wasichana