Mahakama ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachilia huru Dkt. Wilbord Slaa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP kueleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Dkt. Slaa alishtakiwa kwa kuchapisha taarifa za uongo kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, na leo Februari 27, 2025 wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema amewasilisha nia ya DPP mbele ya Hakimu Mfawidhi, Franco Kiswaga.

Wakili Mrema alieleza mahakamani hapo kuwa DPP ameamua kutoaendelea na shauri hilo kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Picha: Rais Samia akiwa na Wanafunzi wa Shule Muheza