Familia ya Mfanyabiashara wa Mafuta ya kula Wilayani Babati Mkoani Manyara, Bashiru Hamis, anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliojifanya kuwa wateja wake na kutokomea naye kusikojulikana wameiomba Serikali na Jeshi la Polisi kuwasaidia, ili ndugu yao aweze kupatikana na kurejea kwenye jukumu yake ya kila siku.
Ndugu wa Mfanyabiashara aliyetekwa wamesema kuwa ndugu yao alipigiwa simu na watu waliojifanya wateja wa mafuta ya kula alipowafata walipo ndipo walimuingiza kwa nguvu kwenye gari na kuondoka naye.
Dereva wa bodaboda aliyembeba Mfanyabiashara huyo siku ya tukio, amesema Mfanyabiashara huyo alipigiwa simu na watu waliojifanya kuwa ni wateja wake na kumtaka awapelekee mafuta ya kupikia jumla ya lita 40
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kija Mkoyi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema hatua walizochukua ni pamoja na ufuatiliaji wa tukio hilo.