Serikali kupitia mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania umeongeza chanzo kipya na endelevu cha mapato ya Mfuko kinachotozwa katika vibebeo tupu vya Kazi za Sanaa (Tozo ya Hakimiliki).

Hayo yamebainishwa hii leo Februari 28, 2025 jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, Nyakaho Mahemba wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya utendaji wa Mfuko huo, katika kipindi chake cha miaka minne.

Amesema, “kupitia chanzo hichi, Mfuko hupata gawio la asilimia 10 ya mapato yote yanayokusanywa na Chanzo hiki kimeanza kutekelezwa Mwezi Septemba, 2023.”

“Vilevile bajeti ya mfuko imeendelea Kuongezeka katika kila mwaka wa Fedha ambapo katika mwaka wa fedha 2023/24 bajeti ya Mfuko iliyoidhinishwa ilikuwa ni shilingi bilioni 1.6 ambapo katika mwaka wa fedha 2024/25 bajeti imeongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 3. na kiasi kilichoongezeka ni Shilingi  Bilioni 1.4ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 87.5,” amesema Mahemba.

Ameongeza kuwa, Mfuko unatoa mikopo kwa kushirikiana na Benki ya CRDB na NBC. Lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma, wakitumia utaalamu na uzoefu wao katika eneo la utoaji wa mikopo, usimamizi wa marejesho pamoja na ufuatiliaji wa miradi iliyowezeshwa.

Mahemba amesema, Mfuko umefanikiwa katika kutoa Mikopo yenye thamani ya Shilingi 5,250,070,500.89 kwa miradi 359 ya Sanaa iliyozalisha jumla ya ajira 497,213, Mchanganuo wa maeneo ya miradi ya iliyowezeshwa ni muziki      (miradi 78), filamu (miradi 90), maonesho (miradi 65), Ufundi  (miradi 103) na Lugha na Fasihi (23).

Mikoa iliyofikiwa ni 18 ambayo ni Dar- Es Salaam, Arusha, Morogoro, Pwani, Geita, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Kagera, Mara, Shinyanga, Tabora, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Simiyu, Kigoma na Katavi.

Muhtasari wa uwezeshaji uliofanyika Mfuko umetoa mikopo yenye thamani ya shilingi 1,246,215,189 kwa miradi ya 78 ya muziki kiasi hiki kimetekeleza katika Kununua vifaa vya kisasa kwa studio 42 za kuzalishia muziki ambapo uwepo wa studio hizi umesaidia kuondoa adha na gharama kwa wanamuziki kuzalishia kazi zao nje ya nchi,” amesema Mahemba

Amesema Studio hizo za kisasa zimewahamasisha wasanii mbalimbali kutoka nje ya Nchi kuja nchini kwetu kwa ajili ya kuzalisha kazi zao,Hivyo, zimekuwa ni chanzo cha mapato ya fedha za kigeni na kuongeza ujuzi, kubadilishana uzoefu na wasanii nchini.

Picha: Rais Samia ndani ya Uwanja wa Mkwakwani
Harusi ni siku moja, ila ndoa ni maisha yako yote: Tafakari