Mazungumzo kati ya Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky na Rais Donald Trump wa Marekani yamevunjika baada ya kutokea kwa mabishani makali yaliyokati yao.
Mabisha hayo, yalipelekea Zelensky kuondoka katika Ikulu ya White House, huku Trump akichapisha kwenye mitandao yake ya kijamii akidai Zelensky aliidharau Marekani katika Ofisi yake ya Oval.
Amesema Kiongozi huyo wa Ukraine anaweza kurejea akiwa tayari kwa amani, akidai Ukraine italazimika kufanya makubaliano katika mapatano na Moscow.
Hata hivyo, Zelensky alisisitiza kwamba haipaswi kuwepo kwa makubaliano na kiongozi “muuaji” (Vladimir Putin), wa Urusi.