Kupitia Wizara ya Afya. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, imewataka raia wake kujitokeza kutoa damu, kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji katika Miji ya Goma na Bukavu.
Hatua hiyo, inakuja kufuatia ripoti ya vifo vya watu 8,500 na wengine zaidi ya 5,000 kujeruhiwa tangu waasi waiingie katika mji wa Goma, idadi ambayo inahofiwa kuwa huenda ikaongezeka.