Wanawake wa Kanisa la TAG Kyarunyonga Kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba wamemshukuru, Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupatiwa mikopo ya asilimia 10 inayowawezesha kupata maendeleo.

Wameyasema hayo leo Machi Mosi, 2025 wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo katika kuelekea siku ya Wanawake Machi 8.

Wamesema, wameshuhudia mageuzi makubwa katika nyanja mabalimbali zikiwemo za kisiasa kiuchumi na kijamiii na mikopo hiyo imefanikiwa kuwainua kimaisha kupitia familia zao na mpaka sasa wanaendelea kujivunia.

“Tunampongeza Mhe Rais kwa kuboresha huduma za afya elimu na uchumi kwa wanawake na vijana na tunampongeza kwa kuleta mikopo isiyokuwa na riba ikiwa maalumu kwa ajiri ya wanawake vijana na wenye ulemavu na kujenga shule maalumu za wasichana kwa kila mkoa ili kupanua wigo wa elimu kwa wasichana” amesema Mratibu mafunzo Petrida.

Katibu Tawala Wilaya ya Bukoba, Proscovia Mwambi ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa amewapongoza waandaji wa semina hiyo yenye lengo la kujenga uelewa wa  wanawake pamoja na wasichana.

Amewataka wasikate tamaa wakati wanapo hitaji kutimiza ndoto zao na kutumia fursa hiyo kuwataka washiriki kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Vijana wa kike tumieni fedha mnazopata katika uwekezaji - Bi. Mlawa
REA yaendeleza usambazaji Mitungi ya Gesi kwa bei ya ruzuku Tanga