Watu wawili wamefariki maisha katika matukio mawili tofauti Mkoani Morogoro ambapo mmoja kwa kujinyonga akiwemo Nungu Nassoro (25) aliyefariki kwa kujinyonga kidaiwa kuwa msongo wa mawazo.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Morogoro, Alex Mkama iliyotolewa hii leo Machi 2, 2025 imeeleza kuwa  Nungu ambaye mfanyabiashara na mkazi wa Kata ya Lukobe, Wilaya na Mkoa wa Morogoro alikutwa amekufa kwa kujinyonga akitumia kamba ya katani kwenye mwembe wa nyumbani  kwake.

Rukio hilo, lilibainika mapema Machi 1, 2025 katika Mtaa na Kata ya Lukobe, Manispaa ya Morogoro huku uchunguzi wa awali ukibaini kuwa chanzo kujiondoa uhai ni msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha.

Katika tukio pili, usiku wa kuamkia Machi 2, 2025 katika Kituo kikuu cha mabasi cha Msamvu, Magnus Simon Timoth Mkinga (22), Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu cha Jordan mkazi wa Kipera, Mkoani Morogoro alizidiwa ghafla na kujilaza chini mbele ya dada yake aitwaye Anna Osward Mbonde (42), Mkazi wa Kibaha wakati wanasubiri usafiri kwenda Mbinga mkoani Ruvuma, kwa ajili ya matibabu.

Juhudi za kumfikisha Hospitali zilifanywa na Polisi, lakini alipofikishwa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro ilibainika kuwa tayari amefariki huku uchunguzi wa awali ukionyesha kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi.

Wagombea NLD mguu sawa kuelekea uchaguzi Mkuu 2025
Vijana wa kike tumieni fedha mnazopata katika uwekezaji - Bi. Mlawa