Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam imekwishaanza kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za DMDP awamu ya pili katika Wilaya zote za Ubungo, Ilala, Kinondoni , Temeke na Kigamboni.
Hayo yamethibitishwa na Meneja Tarura Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geofrey Mkinga wakati akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri wa barabara cha mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa utekelezaji wa miradi ya DMDP umekwishaanza na baadhi ya wakandarasi wapo saiti.
” Miradi ya DMDP iliyosainiwa imekwishaanza toka tarehe 15 mwezi Januari mwaka huu na sasa hivi wakandarasi wote wako ‘site’ wanafanya kazi za awali za uondoaji miuondombinu ya Tanesco na Dawasa ili mradi ukianza kusiwe na usumbufu,” amesema Mhandisi Mkinga.
“Hatua nyingi za awali za kimikataba zimefika mwisho sasa tumeingia katika utekelezaji hivyo ni jambo la lazima kuondoa miundombinu mingine ili tuweze kuweka mitambo barabarani,” aliongeza
Hata hivyo, amearifu kuanza kwa ukarabati wa maeneo ambayo yaliathiriwa na mvua za El Nino pamoja na utekelezaji wa miradi midogo midogo katika mkoa huo.

Wanaume watambue nafasi zao katika kulinda familia - Dkt. Gwajima
Vikundi 60 Wilayani Ilemela vyanufaika na mkopo wa Bilioni 1