Licha ya kuimarishwa kwa miundombinu katika sekta ya afya Nchini, bado ipo changamoto ya upungufu wa wataalamu wa afya, hali inayochangia ongezeko la vifo visivyo vya lazima kwa Wanawake na watoto wachanga.
Hayo yamebainishwa na Mwakilishi wa Wanawake, Salome Cherehani katika kongamano maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani kwa kanda ya Ziwa, lililofanyika wilayani Bukombe Mkoani Geita.

Noella Nyirabihogo/Global Press Journal

Aidha, kupitia Kongamano hilo, pia amesifu jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uanzishwaji wa majukwaa ya wannachi kiuchumi, ili waweze kuwa na lengo moja la kupata fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo mikopo isiyo na riba na ile ya riba nafuu.
Amesema, uwepo wa fursa ya madini umewezesha wanawake kujipatia kipato na kujiimarisha kiuchumi na kuchangia kwenye pato la Taifa, ingawa bado wanawake wanaojishughulisha na uchimbajiwa madini wanakutana na changamoto ya ukosefu wa vifaa, hali inayowafanya kuingia ubia na wanaume na matokeo yake hupata mapato kidogo.

Ladi Kwali: Mfinyanzi aliyepewa heshima ya kipekee Nigeria
Geita: Bilioni 1.5 zimetolewa kwa vikundi 63 vya Wanawake - RC Shigela