Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Steven Wasira amevitaka vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika visisahau shabaha yao ya kukomboa nchi zao kuwa ni sambamba na kuziongoza nchi zao.na kuvitaka vibadili mbinu za kuongoza na visikubali kuyumbishwa na mabadiliko ya dunia yanayotaka kuwatoa kwenye malengo.
Wasira ameyasema hayo katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Mjini Kibaha wakati akifungua mafunzo kwa viongozi wa vyama hivyo vilivyoshiriki katika harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika.
“Mabadikiko ni mengi duniani lakini yasivitoe vyama vyetu kwenye shabaha yake ya msingi ambayo ni kuziongoza nchi zao na kuhakikisha maisha bora na mazuri kwa wananchi huu ndiyo msingi wa vyama hivi,” alisema Wassira.
Ameongeza kuwa, hiyo ndiyo misingi iliyowekwa na waasisi wa mataifa hayo ambayo yalipigania Uhuru wa nchi zao na kuacha misingi imara ambayo inapaswa kufuatwa.
Wasira alisema Mafunzo hayo yana lengo la kupeana mbinu za kuhimarisha vyama hivyo sita ikiwemo CCM ambapo aliwataka viongozi hao wakubali kwenda na wakati na watamgue mabadiliko yanatokea lakini yasiwakumbe wakasahau shabaha iliyokomboa Afrika kwani walipigania uhuru wa jamii iliyokuwepo na vizazi vinavyokuja.
“Na kwasababu vizazi vinavyokuja vinabadilika kunakuwa na vijana wengi zaidi na mifumo ya siasa inabadilika Kutoka chama kimoja kwenda vyama vingi kwahiyo ni lazima kutafuta mbinu ambayo itavifanya vyama hivi vijihimarishe kuanzia chini zaidi visiwe ni vyama vya watu wa chache ilivihakikishe vinaendelea kuongoza Nchi zao,” aliongeza.
“Mbinu ya kuendelea kuongoza nchi zao ni kuhakikisha mabadiliko yoyote ya dunia haiviyumbishi pamoja na kwamba lazima washirikiane na Dunia nyingine lakini wasifanye mabadiliko yakawatoa kwenye shabaha yao maana dunia Ina mambo yake vile vile ikiwa ni.pamoja.na zipo nchi zisizotaka kuona nchi hizo za vyama vya ukombozi vikiendelea kutawala,” alibainisha Wasira.
“Kuna baadhi ya nchi duniani haziipendi kuona vyama hivi vinaendelea kuongoza ambapo wao wanaona demokrasia ni kuviondoa vyama hivyo madarakani pamoja na CCM na ndio maana mara nyingi nimekuwa nikiwauliza tulipatana wakati wa uhuru kwamba CCM tutakaa madalakani kwa muda gani ndio tena tuwape nani Bali sisi tunashabaha ya kuongoza muda mrefu” alise Mabadiliko yanatokea lakini shabaha inabaki ile Iie ya kuhakikisha watu wetu katika nchi hizi na katika tawala za vyama hivi wanapata maisha mazuri hiyo ndio shabaha ya msingi na shabaha hiyo haina mwisho huwezi kusema Maisha sasa yametosha”. ma Wassira
Kwa upande wake Katibu wa masuala ya siasa uhusiano wa kimataifa na Halmashauri Kuu ya CCM – NEC, Rabia Hamidu alisema kuwa nchi hizo zinapaswa kuonyesha umoja wao ili kuzisaidia nchi za Afrika.
Aidha aliwataka washiriki hao kujifunza lugha ya kiswahili ambacho ni lugha yenye asili ya barani Afrika.
Naye Naibu Mkurugenzi wa idara ya masuala ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na idara ya kimataifa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mkuu wa ujumbe wa IDPC Zhang Yanhong alisema kuwa ni jambo zuri kwa ushirikiano wa vyama hivyo sita na CPC.
Mkuu wa Shule ya Mwalimu Julius Nyerere, Prof. Marcelina Chijoriga alisema wanatoa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya siasa, taasisi za umma na serikali pamoja na taasisi za watu binafsi.
Alivitaja vyama hivyo vilivyoshiriki katika harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika kuwa ni pamoja na ANC cha Afrika kusini, FRELIMO cha Msumbiji, NPLA cha Angola, SWAPO cha Namibia, ZANU PF cha Zimbabwe na CCM kwa kushirikiana na chama Cha kikomunisti Cha nchini China CPC.
Alisema Mafunzo hayo yanawashiriki 90 ambapo Kila chama kimetoa washiriki 15 na Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tisa.