Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume, amesema kuwa Mradi wa WARSH umeleta maboresho makubwa katika upatikanaji wa huduma za afya msingi nchini.
Dkt. Mfaume ametoa kauli hiyo alipotembelea Zahanati ya Kijiji cha Manyata, wilayani Kongwa, wakati wa ziara shirikishi ya usimamizi wa huduma za Afya, Lishe, na Ustawi wa Jamii katika Mkoa wa Dodoma.

“Serikali ilitenga zaidi ya Sh.Bilioni 2.16 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na matundu ya vyoo, mifumo ya maji, na vichomea taka,” amesema Dkt. Mfaume.
Aidha, ameeleza kuwa ili kuboresha usafi na upatikanaji wa maji katika vituo vya afya, Serikali kupitia fedha za Benki ya Dunia na mapato ya ndani, inatekeleza programu ya utoaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira vijijini katika mikoa 25.