Afarah suleiman, Mbulu – Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, ameongoza maadhimisho ya siku ya wanawake Mkoa wa Manyara ambapo kimkoa yamefanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Flatei Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ikiwa nikuelekea ambayo kitaifa madhimisho Hayo yanafanyika Machi 8, 2025 jijini Arusha.
Akizungumza na Wanawake katika maadhimisho hayo RC Sendiga ameeleza lengo la maadhimisho hayo ikiwa ni kutoa fursa kwa Kwa wanawake katika kupima mafanikio yaliyofikiwa kimaendeleo, kuhamasisha usawa wa kijinsia na haki kwa wanawake na kuimarisha hali ya uchumi, kisiasa na kijamii.
Sendiga ameeleza kuwa katika Mkoa wa Manyara inaonyesha kuwa kundi la Wanawake na wasichana, limekua likiathirika kutokana na vitendo vya ukatili wa Kijinsia, kutokupewa haki ya kupata elimu kwa watoto wa kike, kunyimwa haki ya kumiliki ardhi au mali katika familia, usawa katika mgawanyo wa madaraka, na kukosa uhuru wa kuwa sehemu ya maamuzi.
“Tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita na wadau mbalimbali kwa Jitihada mbalimbali zilifanyika kuondoa vitendo vya ukatili na kuleta usawa wa kijinsia, kwa kuwa kuwajengea uwezo watoto na Wanawake pamoja na makundi mbalimbali katika jamii kubaini viashiria vya ukatili na kutolea taarifa, na utoaji wa mikopo ya asilimia kumi na isiyo na riba na yenye masharti nafuu ili kuweka mazingira rafiki ya makundi yote kupata huduma bora na kujikwamua kiuchumi,” amesema RC Sendiga.
Akiwa Katika madhimisho hayo Sendiga, amepata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Wajasiriamali pamoja na Banda la wakala wa maji safi na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na kujionea namna wanawake wanavyofanya shughuli za uzalishaji maji pamoja na kutoa vyeti vya pongezi, tuzo, hati za ardhi na yeye kupata tuzo ya mwanamke kinara Mkoa wa Manyara.
Aidha Sendiga, amewapongeza Wanawake wa mkoa wa Manyara kwa kufanya shughuli mbalimbali katika wiki hii ya maadhimisho (tarehe 1 hadi 4) kama kutembelea watoto wenye mahitaji maalumu , wagonjwa,wafungwa na kutoa elimu ya usawa wa kijinsia na ulinzi wa mtoto kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Kauli mbiu ya siku ya wanawake Duniani kwa mwaka 2025 ni “Wanawake Na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezezeshaji.”