Kibaha Mke wa Mbunge wa Kibaha Mjini Mkoani Pwani, Selina Koka amewataka Wanawake Wilayani Kibaha kuzingatia malezi na makuzi bora kwa watoto wao hali itakayowezesha kupata viongozi bora watakaolitumikia taifa kwa kufuata misingi na tamaduni za nchi miaka ijayo.

Amesema kuwa iwapo watoto watalelewa kwa kufuata maadili mema watakuwa na msaada mkubwa kwa jamii ikiwemo kushiriki kuleta maendeleo kupitia shughuli halali.

Ameyasema hayo leo hii leo Alhamisi Machi 6, 2025 alipokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Mjini Kibaha Mkoa wa Pwani.

Mke wa Mbunge wa Kibaha Mjini, Selina Koka wakati akitembelea bidhaa za Wajasiliamali Wanawake wa Mji wa Kibaha Mkoani Pwani katika Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika leo Alhamisi Machi 6, 2025.

“Niwaombe wanawake tuwalee watoto wetu kwa kuzingatia maadili mema na kuwa na nidhamu hiyo itawajengea nidhamu na kuwa na maaadili mema na kuwa viongozi bora miaka ijayo” amesema.

Amesema kuwa viongozi waliopo sasa wanaotekeleza majukumu yao kwa kufuata misingi bora na sharia za nchi walifunzwa na wazazi wao na wakashika maadili mema hivyo katika kuendeleza hayo kuna kila sababu wazazi kutimiza wajibu wao katika malezi bora kwa watoto wao.

“Ili kufikia hilo wanawake tunapaswa kujikita kwenye kazi halali ili hata watoto wetu wajionee kuwa hata matunzo tunayowapa pesa zake ni matokeo ya kazi wanazoziona amesema.

Wakizungumza baada ya maadhimisho hayo baadhi ya washiriki wametaja changamoto zinazowakabili ni ukosefu wa masoko ya uhakika juu ya bidhaa wanazozalisha jambo ambalo linasababisha kushindwa kupiga hatua kiuchumi.

“Changamoto zilizopo kwa sasa ni ufinyu wa masoko tunazalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni,batiki na viatu lakini kinachoturudisha nyuma ni masoko tunaiomba serikali iliangalie hili” amesema.Mariam Simbeye

Evelina Ndalu amesema kuwa kinachosababisha kukosa wateja ni asilimia kubwa ya wanawake kuzalisha bidhaa za aina moja huku kukiwa hakuna masoko ya uhakika hivyo kujikuta wanabaki kugombea wateja.

“Changamoto kubwa ni kwamba asilimia kubwa ya wanawake tunazalisha bidhaa za aina moja ukitengeneza sabuni na vikoi ukienda kwa jirani naye utamkuta anatengenza bidhaa kama ya kwako sasa hapo mteja atakuwa nani?iameshoji.

Amesema kuwa wakati umefika ambao wanawake wanapaswa kuongeza ubunifu na kujiongezea ujuzi hasa katika kuzalisha bidhaa za aina tofautitofauti ili kuwa na wigo mpana wa kupata masoko tofauti na ilivyo sasa ambapo wanagombea wateja.

Serikali kujenga mtandao mkubwa wa  Mabomba ya Gesi - Dkt. Biteko