Saulo Steven – Manyara.
Katika kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Manyara, Regina Ndege akiambatana na Mbunge wa jimbo la mbulu vijijini, Flatei Massay wametembelea Kituo cha Afya katika Halmashauri ya Mbulu na kukabidhi misaada kwenye wodi ya wazazi ikiwemo mashuka, sabuni, mafuta, na mahitaji mengine muhimu.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vitu hivyo kwa akina mama hao kwenye wodi ya wazazi , Regina Ndege pamoja na Massay wamesisitiza umuhimu wa kuwajali wanawake wajawazito ili kuhakikisha uwepo wa afya bora ya mama na mtoto huku wakiahidi kuendelea kutoa misaada ya namna hiyo kwa kadri watakavyojaliwa na mwenyezi Mungu.
Kwa upande wao baadhi ya akina mama hao waliotembelewa na viongozi hao wakizungumza na Dar24 Media mara baada ya kupake msaada wa vitu hivyo kutoka kwa viongozi hao weshukuru kwa msaa huo huku wakipongeza hatua hiyo na kuitaja kuwa ni ya huruma na mshikamano na upendo mkubwa kwao kutoka kwa wabunge hao.
Ikumbukwe kuwa hayo yanajiri ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo machi 8 ya kila mwaka ,na kwa mwaka huu 2025,kitaifa yataadhimishwa jijini Arusha huku Mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.